Mtu Wa Kwanza Kuzungumza Juu Ya Fiqh-ul-Waaqi´ Leo

Jambo hili - yaani Fiqh-ul-Waaqi´ (uelewa wa kisasa) - ni jipya. Kutokana na ninavyojua mtu wa kwanza kulizungumza leo ni Sayyid Qutwub katika kitabu chake "Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan" katika Suurah "Yuusuf" katika mnasaba wa maneno ya Allaah (Ta´ala):

قَالَ اجْعَلْنِي عَلَىٰ خَزَائِنِ الْأَرْضِ ۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٌ
"Akasema: "Niweke nisimamie hazina ya nchi, hakika mimi ni mhifadhi mjuzi."" (12:55)

Hataki Kuzaa Sana Kwa Ajili Ya Kupata Muda Wa ´Ibaadah

Swali: Kuna mwanaume ana watoto wane na anasema kuwa anataka kusitisha kizazi na atosheke na watoto alionao ili apate muda wa kutosha wa kumuabudu Mola Wake kwa sababu kuzaa watoto wengi kunasumbua. Je, anapata dhambi kwa kufanya hivo au hapana?

Jibu: Mtazamo huu ni mpungufu. Kuwalea watoto ni katika kumtii Allaah. Watoto wakiongoka kupitia mikono yako watakunufaisha sawa katika hali ya uhai na ukishakufa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Katika Hali Hii Naweza Kuikata Swalah Yangu Na Kujiunga Na Mkusanyiko?

Swali: Nimekuja kuswali hapa nikakuta swalah tayari imekwisha ambapo nikawa nimeswali peke yangu. Katikati ya swalah kumekuja kundi la watu na wakakimu swalah. Katika hali hii nifanye nini pamoja na kujua kuwa nimeshaswali rakaa´ moja peke yake?

Jibu: Mtu akiingia katika swalah peke yake na kukataka kuswaliwa mkusanyiko mwingine, katika hali hii ana khiyari baina ya mambo matatu:

La kwanza: Anaweza kuendelea na swalah yake, kwa kuwa ni mwenye kupewa udhuru.

La pili: Anaweza kuikata swalah yake ili ajiunge na mkusanyiko.

Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kumwingilia Mke Kwenye Matiti

Swali: Nilipokuwa nastarehe na mke wangu shaytwaan alinishawishi na nikamjamii kifuani mwake mpaka nikawa nimemwaga, kitendo ambacho kinanifanya sina raha. Naomba unijibu hilo na ni ipi kafara ya hilo?

Jibu: Kinachotakikana ni mtu kutumia kila kitu kama ipasavyo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ
"Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo." (02:223)